Dodoma FM

Vumbi lahatarisha afya za wakazi Miganga

31 July 2024, 6:52 pm

Picha ni barabara ya Mtaa huo wa Miganga ambapo gari linapopita huacha vumbi ambalo huishia katika makazi ya watu. Picha na George John.

Eneo hili la Miganga lipo mita 600 tu kutoka stesheni ya SGR, je, serikali haioni changamoto hii na  kuwasaidia wananchi hawa ambao wanaona wametelekezwa?.

Na Mindi Joseph.

Wakazi mtaa wa Miganga wamelalamika kuathirika kiafya kutokana na adha ya vumbi inayosabishwa na kubomolewa kwa barabara kwa ajili ya ujenzi wa daraja la SGR.

Matumaini yamepotea kwa wakazi hao ambao wamezungumza na Dodoma TV wanasema serikali imeshindwa kuwajengea kipande hicho kwa kiwango cha lami na wao kuendelea kuathirika kiafya kwa kuugua vifua na macho.

Sauti za wananchi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Miganga Ludovick Chogwe anasema pamoja na jitihada za kufika mamlaka husika Tanroad na upande wa SGR hakuna kinachofanyika.

Sauti ya Bw,Ludovick Chogwe.
Picha ni barabara ya Mtaa huo wa Miganga ambapo gari linapopita huacha vumbi ambalo huishia katika makazi ya watu.Picha na George John.

Je, vumbi lililochangannywa na saruji lina athari gani kwa afya ya binadamu? Dkt. Damas James kutoka Hospital ya St. Livingstone anaeleza.

Sauti ya Dkt Damas James .

Nini hatima ya wananchi hawa licha ya Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa kufika eneo hilo na kutaka Tanroad na SGR kukaa meza moja lakini imeshindikana?.

Sauti ya Mh.Innocent Bashungwa.