Dodoma FM

RC Senyamule: Maonesho ya nanenane Dodoma yatakuwa ya kipekee

30 July 2024, 6:46 pm

Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemery Senyamule. Picha na Mkoa wa Dodoma.

Mkuu wa Mkoa ametumia nafasi hiyo kuwaalika watu kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi kushuhudia upekee wa maonesho hayo.

Na Seleman Kodima.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewahakikisha wakazi wa Dodoma kuwa maonesho ya Nanenane kitaifa yatakayofanyika Dodoma yatakuwa ya Upekee wa aina yake.

Hayo ameyasema leo wakati akizungumza katika kipindi cha The Morning Power Show kinachorushwa na Dodoma tv,ambapo Mkuu wa Mkoa ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha Watu kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi kushuhudia upekee wa Maonesho hayo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa

Aidha Mkuu wa mkoa wa Dodoma amewataka wakazi wa Dodoma kutumia fursa zinazopatikana katika kituo cha Treni ya Mwendokasi kwa ajili ya kujiinua Kiuchumi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa