Dodoma FM

Shule ya Sekondari Bihawana tunu ya kata ya Mbabala

24 July 2024, 5:25 pm

Picha ni moja ya jengo ambalo lipo katika shule ya sekondari Bihawana.Picha na Fahari ya Dodoma.

Yussuph Hassan ameongea na Diwani wa kata ya Mbabala Mh Pascazia Charles Mawala ambapo anaielezea shule hii.

Na Yussuph Hassan.
Shule ya Sekondari Bihawana ni Shule ya bweni inayodahili wanafunzi wavulana wa Kidato cha Tano na Sita tu.

Shule inatoa Elimu ya sekondari ya juu (Advanced Secondary Education) katika tahasusi za CBA, CBG, HGL,PCB na PCM. Ilianzishwa na Wamisionari ya Kipashonisti wa Kanisa katoliki mwaka 1961.

Mwaka 1974 ilichukuliwa na Serikali ambapo ilianza kuendeshwa na Serikali ya Tanzania hivyo Shule hii ni miongoni mwa Shulekongwe nchini.