Dodoma FM

Tunaendelea kuangazia unawajibikaje kuhakikisha msichana aliyejifungua anarudi shule

23 July 2024, 4:16 pm

Vikwazo vya kijamii, kiuchumi na kisaikolojia vinavyoweza kuwa vizuizi vikubwa. Picha na BBC .

Swali letu kuu Je unawajibikaje kuhakikisha msichana aliyejifungua anarudi shule,huyu hapa Mwemezi Makumba meneja wa utafiti na uchambuzi wa Sera kutoka Haki Elimu anaelezea zaidi.

Na Seleman Kodima.
Bado tupo na taasisi ya Haki Elimu katika kuchimba zaidi jambo hili ambapo utakumbuka kuwa Ripoti ya Shirika la Haki Elimu ya mwaka 2024 imetaja sababu zinazoathiri uwezo wa wasichana waliojifungua kurudi shule, ikionyesha jinsi vikwazo vya kijamii, kiuchumi na kisaikolojia vinavyoweza kuwa vizuizi vikubwa.