Dodoma FM

Ujenzi wa kituo cha polisi Chang’ombe kuimarisha ulinzi

19 July 2024, 4:45 pm

Picha ni ujenzi wa kituo hicho cha Polisi Chang’ombe ukiwa unaendelea.Picha na George John.

Kata ya Changombe ina wakazi wapatao elfu 39000 lakini haikuwahi kuwa na kituo cha polisi na kukamilika kwa ujenzi huu kutaendelea kuiweka kata ya changombe katika hali ya usalama.

Na Mindi Joseph.
Ujenzi wa kituo cha Polisi katika Kata ya Chang’ombe Jijini Dodoma umetajwa kuwa mwarobaini wa kukabiliana na vitendo vya uhalifu na kuimarisha ulinzi.

Ni miaka takribani 4 ujenzi huu ulianza kwa nguvu za wananchi ili kuhakikisha Kata ya chang’ombe inakuwa na kituo cha polisi.

Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi huo Abdallah Mohamend anasema kata hiyo haikuwahi kuwa na kituo cha polisi na hiki ni kituo cha kwanza.

Sauti ya Bw. Abdallah Mohamend .
Picha ni kituo hicho ambacho ujenzi wake umedumu kwa miaka minne.Picha na George John.

Katibu kata Ccm Kata ya Chang’ombe Keto Omary anasema ujenzi huu ni muhimu kwani utapunguza vitendo vya uhalifu.

Sauti ya Bw. Keto Omary.

Kwa upande wa wananchi wamezungumzia ujenzi huo.

Sauti za wananchi.