Dodoma FM

Wakazi wa Nzuguni waombwa kuwa wavumilivu kwa siku kumi maboresho ya Tanki la maji

17 July 2024, 5:45 pm

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph akiongea na wakazi wa Nzuguni.

Mhandishi Aron amewaomba wananchi kuhifadhi na kutumia maji kwa uangalifu.

Na Mariam Kasawa
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph amewaomba wananchi wa Nzuguni na maeneo yanayohudumiwa na mradi wa maji wa Nzuguni kuwa wastahamilivu katika kipindi cha siku 10 wakati Mkandarasi akifanya maboresho ya tenki la lita milioni tatu kuanzia kesho tarehe 15 – 25 Julai, 2024.

Mhandisi Aron amesema hayo katika mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Antony Mavunde na wananchi wa Nzunguzi B kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua

Sauti ya Mhandisi Aron Joseph.