Dodoma FM

Maonesho ya nanenane fursa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali

17 July 2024, 4:15 pm

Picha ni Wafanyabiashara wakizungumzia maonesho ya nanenane ambayo kitaifa yatafanyika hapa Mkoani Dodoma . Picha na Fred Cheti.

Kitaifa Maonesho hayo ya wakulima nane nane yanatarajiwa kufanyika katika Mkoa wa Dodoma katika viwanja vya Nzuguni.

Na Fred Cheti.
Inaelezwa kuwa Maonesho ya wakulima Nane nane yamekuwa yakitoa fursa kubwa kwa wajasirimali na wafanyabiashara jijini hapa kutokana na Mkusanyiko mkubwa wa watu katika Maenesho hayo.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wajasirimali na wafanyabishara Jijini Dodoma wakati wakizungumza na Dodoma Tv kueleza wamejipangaje kupokea maonesho hayo na fursa zipi wanazipata katika maeonesho hayo?

Sauti za wajasiriamali.

Kitaifa Maonesho hayo ya wakulima nane nane yanatarajiwa kufanyika katika Mkoa wa Dodoma katika viwanja vya Nzuguni ambapo maandalizi yake yanatajwa kufikia asilimi hizo 70 kama ambavyo anazungumza Mmoja wa wenyeviti wa maandalizi kanda ya kati Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Halima Dendegu.

Sauti ya Halima Dendegu.