Dodoma FM

Wakazi zaidi 14,000 waondokana na adha ya maji Ntyuka

23 May 2024, 4:27 pm

Hapo awali wananchi walilazimika wananunua ndoo ya Maji hadi shilingi mia Tano.Picha na George John.

Kata ya Ntyuka ina Mitaa mitano na wamenufaika na Visima 3 viliyochimbwa katika maeneo yao kwani viwili vinatoa maji na kimoja bado hakijaanza kutoa maji.

Na Mindi Joseph.
Wakazi zaidi ya Elfu 14,000 wa kata ya Ntyuka Jijini Dodoma Wameondokana adha ya maji kufuatia uwepo wa Tanki kubwa la maji na Visima 3.

Kabla ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA kutekeleza miradi hiyo wananchi walikuwa wananunua ndoo ya Maji hadi shilingi mia Tano lakini sasa wananchota maji nyumbani.
Wananchi wa Kata hiyo wameipongeza DUWASA.

Sauti za wananchi.
Picha ni mkazi wa mtaa huo akiongea na Dodoma Tv. Picha na George John.

Kwa upande Diwani wa Kata ya Ntyuka Yona Mambala anasema eneo lake halina tena changamoto ya maji na kinachosubiriwa ni usambazaji wa mtandao wa Maji.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Ntyuka Yona Mambala.