Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuweka mazingira rafiki kwenye suala la hedhi salama

23 May 2024, 3:59 pm

Mzunguko wa siku za hedhi kwa wanawake ni jambo ambalo huwa halizungumzwi hadharani katika jami.Picha na BBC.

siku ya hedhi salama huadhimishwa kila mwaka Mei 28.

Na Mariam Matundu.
Waziri wa afya ameitaka jamii na wadau kuweka mazingira rafiki kwenye suala la hedhi salama ili mwanamke aweze kutimiza majukumu yake bila kikwazo.

Waziri Ummy amesema hayo wakati akitoa tamko kwa uuma kuhusu maadhimisho ya wiki ya hedhi salama ambapo amesema bila hedhi salama hakuna ustawi .