Dodoma FM

Askofu aliye jinyonga azikwa katika viunga vya kanisa hilo

21 May 2024, 3:44 pm

Picha ni Baadhi ya waombolezaji ambao walifika katika mazishi ya Askofu huyo. Picha na Alfred Bulahya.

Askofu Joseph alipoteza maisha may. 16 mwaka huu baada ya kuchukua maamuzi ya kujinyonga.

Na Alfred Bulahya.
Mwili wa aliekuwa askofu mkuu wa kanisa la Tanzania Methodist TMC Askofu Joseph Bundala umezikwa jana katika viunga vya kanisa la Ihumwa alilokuwa akiliongoza.

Askofu Joseph alipoteza maisha may. 16 mwaka huu baada ya kuchukua maamuzi ya kujinyonga huku akiacha ujumbe kuwa sababu za uamzi wa kujinyonga ni kutokana na madeni anayodai na kudaiwa.

Akizungumza baada ya kuupumzisha mwili wa askofu huyo, makamu askofu mkuu wa kanisa la Tanzania Methodist TMC Samweli Nyanza Moze amewataka waumini wa kanisa hilo na jamii kwa ujumla kuwa watulivu wakati vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

Sauti ya makamu askofu mkuu wa kanisa la Tanzania Methodist TMC Samweli Nyanza Moze.