Msukumo mkubwa wa maji wachangia kupasuka kwa mabomba
15 April 2024, 9:34 pm
Duwasa imeendelea kuhakikisha inakabiliana na changamoto ya upotevu wa maji ambao husababishwa na kupasuka kwa miundombinu ya Mabomba ya maji kutokana na presha kubwa ya maji.
Na Mindi Joseph.
Msukumo mkubwa wa maji umetajwa kuchangia Kupasuka kwa miundombinu ya mabomba ya maji Nzuguni na kuchangia upotevu wa maji ambao unaathiri upatikanaji wa huduma hiyo.
Dodoma Tv imezungumza na Kaimu Mkurugenzi wa usambazaji wa maji na usafi wa mazingira DUWASA Mhandisi Benard Rugayi ambapo amesema changamoto hiyo imekuwa ikijitokeza lakini wamekuwa wakichukua hatua za haraka kukabiliana na changamoto hiyo.
James Rioba ni Mhandisi wa Maji kutoka DUWASA anasema wanatimu ya kuhakikisha pindi wanapopokea taarifa za mabomba ya maji kupasuka wanaitatua mara moja na kuhakikisha maji yanawafikia wananchi husika.