Dodoma FM
Km 19 za barabara kujengwa katika mitaa zaidi ya minne Makulu
12 October 2023, 12:40 pm
Tayari wananchi waliopisha ujenzi wa Barabara hizo wameshalipwa stahiki zao.
Na Mindi Joseph.
Kilomita 19 za barabara zinatarajiwa kuchongwa katika zaidi ya Mitaa 4 katika Kata ya Dodoma Makulu kabla ya msimu wa mvua kuanza.
Hii ni kufuatia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami inayounganisha kata 3 ikiwemo kata ya Dodoma Makulu uliogharimu zaidi ya shilingi bilion 10 kukamilika.
Taswira ya Habari imezungumza na diwani wa kata ya Dodoma Makulu Mh. Fadhili Chibago hapa anaeleza kuhusu ujenzi wa barabara hiyo.
Maboresho katika barabara hiyo yanaendelea ikiwemo kuweka alama za watembea kwa miguu ili kuepusha Ajali.