MCT yakiri kukinzana kwa sheria ya matumizi sahihi ya mitandao
28 September 2023, 4:42 pm
Hali hiyo imekuwa ikikinzana na Sheria ya haki ya kupata Taarifa ambayo inatoa wigo kwa wananchi kuwa huru kupata taarifa ambazo hazijazuiliwa kisheria.
Na Seleman Kodima.
Pamoja na Serikali kuhimiza Matumizi sahihi ya Mitandao ya kijamii, Baraza la Habari Tanzania limesema bado kuna kukinzana kwa sheria.
Hii ni kufuatia sheria kuwabana wananchi wenye majukwaa ya mitandao ya kijamii kwa kuwataka walipe gharama ya Shilingi Laki Tano kwa ajili ya Usajili.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Baraza la Habari ilitolewa leo katika kuadhimisha Haki ya upatikanaji Taarifa ambayo huadhimishwa Septemba 28 kila mwaka, imefafanua kuwa kupitia kauli mbiu ya mwaka huu ya Umuhimu wa Mitando katika Upatikanaji wa Taarifa wamekiri suala hilo kushindika kufanyika kwa sababu ya Sheria zilipo nchini.
Aidha taarifa hiyo imeeleza hali ya upatikanaji wa taarifa kwa sasa ambapo kufikia Septemba Mwaka huu Baraza la Habari limerekodi Matukio Mawili ya waandishi kunyimwa taarifa huku matukio mengine yakiwanyima fursa wananchi kupata taarifa kutoka kwenye Vyombo vya habari.
Baadhi ya Matukio hayo ni pamoja na Waandishi wa Habari kutishiwa,kukamatwa na kuzuiwa kwa mijadala inayohusu Dp World.
Hata hivyo Baraza la Habari limetoa Mapendekezo yenye lengo la kufanikisha Haki ya upatikanaji wa taarifa ikiwa ni pamoja mitandano ya kijamii itumike kwa umakini katika kutoka taarifa sahihi na za ukweli,Serikali kuendelea na nia yake kufanyia marekebisho sheria mbalimbali ambazo zinakandamiza Uhuru wa Kujieleza pamoja na uhuru wa vyombo vya habari.
Baraza limeomba Serikali iendelee kusikiliza maoni ya Wadau na kuyafanyia kazi kutazama upya sheria ya EPOCA katika kanuni za mtandaoni ,Sheria ya haki ya kupata taarifa 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandaoni zinafanyiwa marekebisho ambayo yatachangiza upatikanaji rahisi wa taarifa kwa wananchi.