Hombolo Makulu walia na uchakavu wa shule
20 September 2023, 4:45 pm
Mazingira magumu au uchakavu wa miundombinu ya shule pamoja ongezeko la wanafunzi ni moja ya changamoto zinazo ikabili sekta ya elimu.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa mtaa wa Hombolo Makulu wamelalamikia uchakavu wa miundombinu ya shule yao ya msingi hali inayo wakosesha ufanisi walimu na wanafunzi wa shule hiyo
Wamesema kuwa ubora wa mazingira ya shule unaweza kuwa kivutio kikubwa kwa mwanafunzi katika kuongeza morali wa kujifunza pamoja na ufanisi wa kufundisha kwa walimu
Aidha wameongeza kuwa uchakavu wa miundombinu hiyo ya madarasa unapelekea usalama mdogo wa kutunza dhana zao za kujifunzia
Wamesema kuwa kukosekana kwa ukarabati mashuleni unaweza kupelekea baadhi yd watoto kukua kwa kuichukia kutokana na mazingira magumu waliyonayo shuleni
Wiliamu Mkuna mwenyekiti wa mtaa huo amesema changamoto kubwa ni uchakavu wa shule mama ya msingi kutokana na kujengwa kipindi cha miaka ya ukoloni
Mkuna amesema kuwa hata hivyo tayari shule hiyo imetengewa bajeti yake ya kujengwa upya huku akitoa shukrani kwa Serikali kwa ujenzi wa shule ya mfano katika kitongoji cha Maheto