Dodoma FM
Mradi wa maji wa Nzugumi wafikia asilimia 87
19 September 2023, 4:31 pm
Mkoa wa Dodoma unazalisha nusu ya mahitaji ya maji ambapo mahitaji ya maji ni lita Milion 133 kwa siku na yanayozalishwa ni lita milion 67.8 hivyo kuwa na upungufu wa lita Milioni 66.7 kwa siku.
Na Mindi Joseph.
Mradi wa maji wa Nzuguni ambao unatarajia kukamilika mwanzoni mwa mwezi Oktoba umefika asilimia 87 ya utekelezaji wake.
mradi huo ukikamilika utahudumia wananchi wa Nzuguni, Swaswa, Ilazo na Nyumba 300 wapatao 75,000.
Mkurugenzi wa Usambazaji na Usafi wa Mazingira wa DUWASA, Mhandisi Emmanuel Mwakabole anazungumzia mradi huo.
Tenki la ujazo wa lita milioni tatu tayari limefungwa katika mradi mkubwa wa maji Nzuguni.