Bei ya maharage yazidi kupaa sokoni
17 August 2023, 4:19 pm
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ilibainisha bei ya mazao ya chakula ikiwemo maharage imepungua kutoka asilimia 33.5 hadi asilimia 28.3 kwa mwaka ulioshia mwezi Julai 2023 ikilinganishwa na mwaka ulioshia mwezi Juni 2023.
Na Mariam Msagati.
Bei ya maharage imeendelea kupanda katika masoko mbalimbali Jijini Dodoma ikiwemo soko la Majengo pamoja na Sabasaba huku sababu kubwa ikiwa ni uhaba wa bidhaa hiyo kutoka kwa wakulima.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wafanyabiashara wa bidhaa hiyo ambapo wanasema kuwa licha ya bidhaa hiyo kushuka kwa siku za hivi karibuni lakini kwa sasa bei ya bidhaa hiyo imepanda ghafla.
Baadhi ya wananchi pamoja na wafanyabiashara wa chakula wanasema kuwa kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo kunaendelea kuwaathiri hususani katika suala la kupata wateja.