Wilaya ya Kondoa yaagizwa kulipa madeni ya watumishi umma
12 July 2023, 3:05 pm
Halmashauri hiyo imetakiwa kuhakikisha inalipa madeni yote ya watumishi wa umma kabla ya kupokea bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/24.
Na Fred Cheti.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule ameiagiza halmashauri ya Kondoa kuhakikisha inalipa Madeni yote wanayodaiwa na watumishi wa Umma katika halmashauri hiyo kabla ya kupokea fedha za bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/24
Mhe.Rosemary Senyamule amaeyasema hayo wakati akisiriki katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Vijijini kwa lengo la kujadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa serikali katika halmashauri hiyo
Aidha katika hatua nyingine Mh Rosemary ameipongeza halmashauri ya wilaya hiyo ya Kondoa vijijini kwa kupata hati safi Kwa ukaguzi wa hesabu za serikali zinazoishia Juni 30 mwaka 2022.