Mahakama kuu divisheni ya kazi yaahidi kushirikiana na osha
3 May 2023, 5:38 pm
Dkt. Mlyambina amemshukuru Mtendaji Mkuu wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA) kwa kuridhia mpango wa utoaji Elimu kwa Menejimenti ya Mahakama Kuu Divisheni ya kazi.
Na Alfred Bulahya.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Mhe. Yose Mlyambina amesema wataendelea kushirikiana na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ili kuhakikisha watumishi wanatekeleza majukumu yao katika hali ya usalama na afya bora.
Ameyasema hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe, Prof. Joyce Ndalichako katika Uwanja wa Tumbaku Mkoani Morogoro.
Aidha Dkt Mlyambina Amesema wameandaa mkakati wa kupokea elimu kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Usalama na Afya Mahali pa Kazi ambao utahusisha Menejimenti ya Mahakama, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ili kujitathimi na kuzingatia sheria na kanuni za Usalama na Afya mahali pa kazi.