Watu wenye ulemavu wametakiwa kuchangamkia fursa
24 April 2023, 4:28 pm
Kwa Sasa serikali imekuwa ikitoa fursa nyingi ambazo watu wenye ulemavu wanahaki ya kushiriki na kuwataka kuchangamkia kila fursa inayotolewa ikiwemo mikopo ya asilimia 10 ya halamshauri ambayo kundi hilo litapata asilimia 2 .
Na Fred Cheti.
Wito umetolewa kwa makundi ya watu wenye ulemavu nchini kutumia vizuri fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali kwa kundi hilo ikiwemo mikopo kwa ajili ya kujipatia maendeleo.
Rai hiyo imetolewa na Makamu mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya jamii ambae pia ni Mbunge wa viti maalum (CCM) Bi. Riziki Lulida wakati Akizungumza na baadhi ya watu wenye ulemavu alipowatembelea na kuwashika mkono kwa baadhi ya mahitaji katika moja ya ofisi zao zilizopo maeneo ya shule ya sekondari viwandani jijini Dodoma.
Kwa upande wao baadhi ya watu wenye ulemavu katika kituo hicho wameishukuru serikali kwa kuendelea kutengeneza fursa mbalimbali kwa kundi hilo.