Serikali yadhamiria kudhibiti na kutokomeza kifua kikuu
22 March 2023, 3:46 pm
Immelezwa kuwa watu wenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa kifua kikuu(TB) ni pamoja na wale wanaoishi katika makazi duni, Watoto, Wavuvi na wanafunzi wanaoishi bweni.
Serikali imedhamiria kuendelea kushirikiana na wadau katika sekta zote ili kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ifikapo mwaka 2030.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi katika kikao na Makatibu Wakuu wa Wizara kilichofanyika katika ofisi za Waziri Mkuu Jijini Dodoma.
Kwa upande wake Mtaalamu Mshauri kutoka Stop TB Partnership (STP) Bw. Oscar Mukasa wakati akiwasilisha taarifa ya mpango kazi wa kudhibiti Kifua Kikuu amesema watu wenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo ni pamoja na wale wanaoishi katika makazi duni, Watoto, Wavuvi na wanafunzi wanaoishi bweni.
Aidha Bw. Mukasa amewashauri watu wanaoishi katika mazingira Duni kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) kwa kufuata maelekezo yote yanayotolewa na wataalamu wa afya.