LATRA yafafanua usafirishaji wa mizigo ya Abiria
20 February 2023, 2:08 pm
Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kwa mujibu wa kanuni ya 37 ni wajibu wa msafirishaji wa gari la abiria kumsafirishia abiria mzigo wake bure kama hauzidi kilo 20.
Na Mindi Joseph.
Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kwa mujibu wa kanuni ya 37 ni wajibu wa msafirishaji wa gari la abiria kumsafirishia abiria mzigo wake bure kama hauzidi kilo 20.
Akizungumza na Taswira ya habari Ezekiel Emmanuel Afisa Mfawidhi Latra amesema abiria anaposafiri na mzingo ni wajibu wa msafirishaji kusafirisha bure endapo unakidhi viwango.
Kwa mujibu wa kanuni ya 37 ni wajibu wa msafirishaji wa gari la abiria kumsafirishia abiria mzigo wake bure kama hauzidi kilo 20.
Katika hatua nyingine amezungumzia watu wenye ulemavu juu ya vifaa vyao vinavyowawezesha kutembea mara baada ya kushuka katika vyombo vya usafiri.