Wakazi wa Njoge wahofia kuharibika zaidi kwa miundombinu ya barabara msimu wa mvua
19 October 2022, 9:15 am
Na; Victor Chigwada.
Kuchelewa kwa ukarabati wa barabara za kata ya Njoge umewapa wasiwasi wakazi wa kata hiyo wakati wakijiandaa na msimu majira ya mvua
Wakizungumza na Taswira ya Habari baadhi ya wananchi wa kata hiyo wamedai kuwa barabara hizo zimesahaulika hali ambayo inatoa wasiwasi pindi mvua zinapo kuwa zinanyesha kutokana na ubovu wa barabara hiyo
.
Diwani wa Kata hiyo Bw.Abdala Dedu amekiri kukabiliwa na uchakavu huo wa miundombinu ambao bado wanajaribu kufuatilia kwa karibu ili kufanya ukarabati kipindi hiki cha kiangazi
Ameongeza kuwa mwingiliano wa mipango kazi ya Serikali ikiwa ni pamoja na sensa huenda ilikwamisha baadhi ya miradi kuendelea katika maeneo mengi nchini
.
Naye mwenyekiti wa Kijiji Cha Njoge Bw.Peter Mwachahe amesema pamoja na adha hiyo lakini zipo baadhi ya barabara zinazopitika bila tatizo.
.