Dodoma FM

Mtindo wa maisha unaathiri vipi afya ya akili?

8 April 2026, 11:56

Picha ni baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya afya ya akili Mirembe.Picha na Mtandao.

Katika majadiliano haya , tutaangazia jinsi mtindo wa maisha unavyoweza kuathiri afya ya akili .

Afya ya akili ni sehemu muhimu ya ustawi wa jumla wa mwanadamu. Ni hali ya akili kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha, kufikia malengo, na kushirikiana na jamii kwa njia yenye maana na yenye kuridhisha.

Kwa upande mwingine, ugonjwa wa akili unahusisha matatizo ambayo yanaathiri mawazo, hisia, na tabia za mtu, na yanaweza kuathiri uwezo wake wa kufanya kazi za kila siku.