Dodoma FM

Maadhimisho ya Afya na lishe yafanyika Zuzu

31 March 2026, 19:45

Wataendelea kuzingatia utoaji wa elimu ya lishe kwasababu suala la lishe bora ni mtambuka.Picha na Anwary Shaban.

Maadhimisho hayo yalihusisha utoaji elimu ya lishe kuhusu makundi ya vyakula, matunda na mbogamboga, upimaji uzito watoto na wajawazito na pia upishi wa vitendo wa uji ulifanyika ili kuonesha namna bora ya kupika uji wa lishe.

Na Anwary Shaban.

Wananchi wametakiwa kutambua umuhimu wa lishe hasa kwa mama mjamzito na watoto.

Hayo yamesemwa katika maadhimisho ya Afya na Lishe (SALIKI) yamefanyika katika Kata ya Zuzu ambapo elimu ya matumizi ya lishe bora yalitolewa kwa wananchi lengo ikiwa ni kuhakikisha jamii inatambua umuhimu wa lishe kwa ustawi wa afya bora.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kupata elimu hiyo katika Zahanati ya Zuzu, Diwani wa Kata ya Zuzu, mh. Jenista Maringo amesema kuwa upo umuhimu mkubwa wa mama mjamzito na watoto kupata lishe bora ili kutengeneza jamii yenye watu walio na afya bora.

Nae, Afisa Mtendaji wa Kata ya Zuzu, James Hans alisema kuwa wataendelea kuzingatia utoaji wa elimu ya lishe kwasababu suala la lishe bora ni mtambuka na haliepukiki.

Katika hatua nyingine, Muuguzi katika Zahanati ya Zuzu, Juma Nyala alieleza kuwa anayo furaha kuona mwitikio mkubwa wa wananchi kujitokeza kupata elimu hiyo ya lishe.