Dodoma FM

Sera ya maji ya Taifa toleo la 2025 yazinduliwa

31 March 2026, 19:27

Picha ni mkurugenzi wa rasilimali za maji wizara ya maji Robert Sunday wakati wa uzinduzi wa sera ya maji .Picha na Noah Patrick.

Wizara ya Maji kupitia Idara ya Rasilimali za Maji ina jukumu la kuhakikisha mabwawa ya maji na tope sumu (Tailing StorageFacility-TSF) yanakidhi vigezo vya usalama wa mabwawa.

Na Anwary Shaban.

Wizara ya Maji imezindua Sera ya Maji ya Taifa ya mwaka 2002 toleo la 2025 ambayo imeweka msisitizo katika uendelezaji wa rasilimali za maji ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha usalama wa maji kwa Taifa, usalama wa chakula, ukuaji wa uchumi sambamba na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa rasilimali za maji wizara ya maji Robert Sunday wakati akimuwakilisha katibu mkuu wizara ya maji Mhandisi Mwajuma juma katika uzinduzi huo ambapo amesema kuwa Ujenzi wa mabwawa ya maji utawezesha kuvuna maji ya mvua kwa lengo la kuya hifadhi kwa matumizi wakati wa kiangazi lakini pia kuzuia mafuriko ya nayotokana na mvua nyingi.

Sauti ya Robert Sunday.

Aidha amesema kuwa  Wizara ya Maji kupitia Idara ya Rasilimali za Maji ina jukumu la kuhakikisha mabwawa ya maji na tope sumu (Tailing StorageFacility-TSF) yanakidhi vigezo vya usalama wa mabwawa kwa mujibu wa Sheria ya Rasilimali za Maji pamoja na Kanuni za Usalama wa Mabwawa.

Sauti ya Robert Sunday.

Kwa upande wake Domina Msonge ambaye ni mkuu wa kitengo cha usalama wa mabwawa ameeleza maana ya mabwawa na tope sumu kwa lugha nyepesi nakusema kuwa ni mabwawa yanayotumika kuhifadhi tope linalotokana  na uchenjuwaji wa madini

Sauti ya Domina Msonge

Pia amesema kuwa wakati wa ujenzi wa mabwawa hayo ujenzi hufatiliwa ili kuhakikisha mjenzi anajenga kulingana na michoro ya kihandisi iliyothibitishwa kuwa bwawa litakuwa salama.

Sauti ya Domina Msonge