Dodoma FM

Vijana waliopata mafunzo mradi wa AHADI wafanya mahafali

27 March 2026, 17:16

Mahafali hayo yamefanyika jijini Dodoma yakihusisha wadau mbalimbali wa maendeleo, viongozi wa serikali pamoja na vijana.Picha na Anwary Shaban.

Kwa ujumla, mradi wa AHADI unaosimamiwa na TAHEA umeonesha mafanikio makubwa katika kuwawezesha vijana, huku serikali ikiahidi kuendeleza juhudi hizo kwa manufaa ya jamii na vijana.

Na Anwari Shaban.

Shirika lisilo la kiserikali la TAHEA kwa kushirikiana na ufadhili wa Serikali ya Canada kupitia shirika la World Vision Tanzania, limefanya mahafali ya kufunga rasmi utekelezaji wa Mradi wa AHADI kwa vijana waliopata mafunzo kuanzia mwaka 2024 hadi 2025.

Mahafali hayo yamefanyika jijini Dodoma yakihusisha wadau mbalimbali wa maendeleo, viongozi wa serikali pamoja na vijana walionufaika na mradi huo, ambapo lengo kuu limekuwa ni kuwawezesha vijana kiuchumi na kijamii kupitia mafunzo na miradi ya maendeleo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mratibu wa Mradi wa AHADI katika eneo la afya, Situ Muhunzi, amesema mradi huo umeleta mafanikio makubwa kwa vijana kwa kuwapatia elimu mbalimbali pamoja na fursa za kujifunza kwa vitendo kupitia ziara za mafunzo katika maeneo tofauti ikiwemo Chamwino.

Mahafali hayo yamefanyika jijini Dodoma yakihusisha wadau mbalimbali wa maendeleo, viongozi wa serikali pamoja na vijana.Picha na Anwary Shaban.

Kwa upande wake, Mratibu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Elizabeth Kyula, ameipongeza timu ya usimamizi wa mradi wa AHADI kwa mchango wao mkubwa katika jiji la Dodoma, huku akiwataka vijana hao kutumia vizuri vituo vya afya vilivyopo ili kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Mradi huo, Fatuma Kitojo, amewapongeza wahitimu kwa juhudi walizo onesha wakati wa mafunzo na kusisitiza umuhimu wa kuyaendeleza maarifa waliyopata ili kuleta tija katika jamii zao.

Sauti kina.