Dodoma FM

Serikali yatakiwa kuimarisha usimamizi wa miundombinu ya mawasiliano Nchini

25 March 2026, 09:45

Picha ni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati wa ziara ya kikazi mkoani Manyara kukagua ujenzi wa minara mipya ya simu.Picha na UCSAF.

Wananchi wametakiwa kutumia fursa hiyo ya kiteknolojia kujikwamua kiuchumi na kulinda miundombinu hiyo dhidi ya uharibifu.

Na Mariam Kasawa.

Serikali imetakiwa kuendelea kuimarisha usimamizi wa miundombinu ya mawasiliano nchini ili kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa vijijini.

Agizo hilo limetolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati wa ziara ya kikazi mkoani Manyara kukagua ujenzi wa minara mipya ya simu.

Katika juhudi za kuhakikisha huduma bora za mawasiliano zinafika kila kona ya nchi, Kamati ya PAC imepiga kambi mkoani Manyara.

Lengo kuu ni kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UCSAF, Balozi Valentino Mlowola, alianza kwa kutoa tathmini ya utekelezaji wa miundombinu hiyo ya kisasa.

Sauti ya Balozi Valentino Mlowola.
Picha ni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati wa ziara ya kikazi mkoani Manyara kukagua ujenzi wa minara mipya ya simu.Picha na UCSAF.

Baada ya kujionea maendeleo hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Mheshimiwa Devotha Minja, hakuishia tu kukagua, bali alitoa neno la hamasa kwa wakazi wa Kijiji cha Qash.

Amewataka kutumia fursa hiyo ya kiteknolojia kujikwamua kiuchumi na kulinda miundombinu hiyo dhidi ya uharibifu.

Sauti ya Mheshimiwa Devotha Minja.

Kwa upande wao, wananchi wa kijiji hicho wameeleza furaha yao, wakisema kupatikana kwa mawasiliano kutaondoa kero ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za mtandao.

Sauti za wananchi.