Dodoma FM

Wanawake KKKT Mpwapwa wawashika mkono wanawake wanaopitia changato

18/03/2026, 18:16

Picha ni Umoja wa wananawake wa kanisa la kiinjili la kirutheli Tanzania dayosisi ya Mji mpya wilayani Mpwapwa.Picha na Steven Noel.

Wamesema lengo la kutoa msaada huo pia ni kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka machi 8 hivyo wametumia maadhimisho hayo kutoa msaada huo.

Na Steven Noel.
Umoja wa wananawake wa kanisa la kiinjili la kirutheli Tanzania dayosisi ya Mji mpya wilayani Mpwapwa wametoa msaada wa vitu mbalimbali Kwa wanawake wanaopitia magonjwa ya muda mrefu na umaskini wa kipato.

Wakiongea mara baada ya kutoa msaada Katika jumuiya ya waumini Kanisa hilo kata ya Gulwe baadhi ya akina mama wamesema wapo wanawake Wanaopitia changamoto za Maradhi,na changamoto zingine za kimaisha hivyo lazima wasaidiane wenyewe Kwa wenyewe.

Wamesema lengo la kutoa msaada huo pia ni kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka machi 8 hivyo wametumia maadhimisho hayo kutoa msaada huo.

Mwezi march Kila mwaka wanawake wote duniani huungana kushereheke siku ya mwanamke ambapo maadhimisho haya huambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya matendo ya huruma kwa wasio jiweza.

Sauti Kina.