Dodoma FM
Dodoma FM
09/03/2026, 20:56

Kila mwaka mwezi Machi huadhimishwa kama mwezi wa wanawake, ambapo wanawake hupata nafasi ya kutafakari mafanikio yao pamoja na changamoto wanazokutana nazo katika nyanja za kiimani, kiuchumi na kisiasa.
Na Steven Noel.
Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa mkoani Dodoma, Nathan Malima, amewataka akina mama kuto kumuacha nyuma mtoto wa kiume katika malezi kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto katika nyakati hizi.
Mhe. Malima ameyasema hayo wakati wa Siku ya Maombi ya Mama wa Kikristo iliyofanyika wilayani Mpwapwa, ambapo maombi hayo yalifanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Paul lililopo Mpwapwa Mjini.
Amesema kuwa katika kipindi hiki ambacho jamii inapambana na masuala ya ukatili dhidi ya mtoto wa kike, ni muhimu pia kuhakikisha mtoto wa kiume hapuuzwi katika malezi ili kukua katika maadili mema.
Kwa upande wake, muhubiri wa siku hiyo Bi. Neema Rojas amewataka wanawake kuwa wanyenyekevu katika ndoa zao ili kuweza kuokoa kizazi cha sasa ambacho kinakabiliwa na changamoto za malezi ya upande mmoja.