Dodoma FM
Dodoma FM
09/03/2026, 20:17

Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) inayohusika na Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) inasema, lengo ni kusaidia maboresho ya uelewa mpana zaidi wa mapambano dhidi ya biashara na matumizi haramu ya dawa za kulevya duniani.
Na Jerome John.
Jamii mkoani Dodoma imeshauriwa kutojiusisha na utumiaji wa dawa za kulevya au uuzaji kutokana na madhara makubwa yanayoweza kujitokeza endapo ukibainika.
Akizungumza na Taswira ya habari Afisa elimu kutoka mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya DCEA ,Anna Tengia amesema kuna madhara makubwa kwa wale wanaotumia dawa za kulevya,kubadilika kwa tabia,hisia na fikra na kusababisha kufanya matendo ya kikatili au kufanya makosa ya jinai katika jamii.
Aidha amesema kuwa kuna vitendo vinavyofanywa katika jamii ambavyo sio vya kawaida na kupelekea madhara na kufanya mambo hatarishi kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri na kufanya maamuzi unapokuwa umetumia bangi,skanka au heroin na aina nyingine ya dawa za kulevya.
Kwa upande wake mwanasheria Meshack Lyabonga amebainisha kuwa ukipatikana na hatia ya kujiusisha na dawa za kulevya kwa kufanya biashara au kugundulika kuwa mali ulizonazo zimetokana na kujiusisha na dawa za kulevya zitataifishwa na muhusika kufungwa kifungo kulingana na ukubwa wa kosa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.