Dodoma FM
Dodoma FM
06/03/2026, 16:25

Kliniki hiyo ya kutatua kero kwa wananchi itachukua takribani siku tatu na Moja ya dhamira kuu ya serikali nikuhakikisha mwananchi hatembei umbali mrefu kwenda kupata huduma badala yake wamezisogeza taasis zote za kiserikali katika eneo moja ili kutatua kero kwa wananchi.
Na Anwary Shaban.
Halmashauri ya jiji la Dodoma imeelekeza kila kata kutenga kiasi cha shilingi milioni mia moja na hamsini kujenga masoko kwa ajili ya wajasiriamali .
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri katika kliniki iliyo zikutanisha taasisi mbalimbali za kiserikali katika kutatua kero za wananchi mbalimbali ikiwa ni mafanikio ya siku 100 za Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemery Senyamule ameizungumzia cliniki iliyo zikutanisha taasis mbalimbalimbali za serikali kutatua kero za wananchi ambapo amesema wakazi wa Dodoma wanapaswa kuzitumia siku hizi zilizo tengwa kwaajili ya kutatuliwa kero zao.
Mh.Senyamule ameeleza kuwaa mpango wa utekelezaji wa kero za wananchi ambayo inafahamika kwa kauli mbiu isemayo Kero yako wajibu wangu ilianza kutekelezwa tangu mwaka 2023 na bado unaendelea kufanyika .