Sheria mpya ya manunuzi yasaidia kuboresha manunuzi pamoja na sekta ya ugavi
Sheria mpya ya manunuzi yasaidia kuboresha manunuzi pamoja na sekta ya ugavi
26/02/2026, 12:50
Picha ni katibu mtendaji wa mamlaka ya rufani ya zabuni za Umma (PPAA) Ndugu James Sando wakatiakizungumza na waandishi wa Habari Dodoma.Picha na Bennard Filbert.
Ameongeza kuwa jumla ya rufaa 26 zimewasilishwa na kushughulikiwa na mamlalaka ya rufani ya zabuni za Umma.
Na Bennard Komba.
Imeelezwa kuwa kutungwa upya kwa sheria ya manunuzi serikalini 2024/2025 imesaidia kuboresha manunuzi Pamoja na sekta ya ugavi Pamoja na kuunga nisha maeoneo mbalimbali ukiringanisha na hapoawali.
Haya yameelezwa na katibu mtendaji wa mamlaka ya rufani ya zabuni za Umma (PPAA) Ndugu James Sando wakatiakizungumza na waandishi wa Habari Dodoma.
Amesema maboresho hayo yamefanya kuimarika kwa mifumo ya usimamizi wa manunuzi na ugavi ikiwepo kupungua kwa muda wa kushughulikia malalamiko na rufaa zinazo tokana na manunuzi ya ummaa.
Sauti ya Bw. James Sando
Kadhalika amesema hadi hivi sasa malalamiko 660 yamewasilishwa na kushughulikiwa na taasisi nunuzi jambo lilionesha muitikio chanya.
Sauti ya Bw. James Sando
Mamlaka ya rufani ya zabuni za Umma (PPAA) ni mamlaka huru ya Serikali ya Tanzania iliyo anzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma (Public Procurement Act) kwa lengo la kushughulikia rufaa zinazotokana na michakato ya zabuni za umma.