Dodoma FM
Dodoma FM
19/02/2026, 17:25

Shirika la water mission tayari limeanza kusambaza mabomba ya maji katika vitongoji vya kijiji hicho.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Kijiji cha Mjelo kata ya Handali Jijini Dodoma wamepata tumaini la kuondokana na adha ya maji baada ya shirika la water mission kusambaza mabomba ya maji katika vitongoji vya kijiji hicho.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mjelo Bw.Emmanuel Tanaga ameeleza namna walivyopokea mradi huo wa usambazaji maji kupitia shirika la water mission ambapo amesema mradi huo utarahisisha huduma ya maji kijiji hapo.
Nao baadhi ya wakazi wa Mjelo wamesema wanatamaini kupata huduma ya maji nyumbani kwa kuvuta mabomba hayo ya maji kwani wameteseka muda mrefu kutembea umbali mrefu na kupanda foleni ili kupata huduma hiyo ya maji.