Dodoma FM

Wakazi wa Miyuji walalamikia ubovu wa barabara za mitaani

19 February 2026, 4:54 pm

Mvua zinazo endelea kunyesha jijini Dodoma zimedaiwa kuharibu barabara hizo hasa eneo la miyuji.Picha na mtndao.

Mhe Ringo amewaonya wananchi ambao wanajenga uzio na kuziba mitaro ya maji kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwani.

Jerome John.

Wananchi wa kata ya Miyuji halmashauri ya jiji la Dodoma wametakiwa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mvua baada ya kulalamikia ubovu wa miundombinu ya Barabara.

Wito huo umetolewa na diwani wa kata hiyo Mhe Ringo Iringo akizungumza na Taswira ya Habari baada ya kutafutwa kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu ubovu wa barabara katika kipindi hiki cha mvua na kusababisha baadhi  ya shughuli za kimaendeleo kukwama.

Sauti za Wananchi.

Aidha diwani huyo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo kwa baadhi ya mitaa na kusema kuwa jitihada zinafanyika kwa kushirikiana na Tarula ilikuweza kubaini Barabara zote zenye changamoto na kuzifanyia marekebisho.

Sauti ya Mh. Ringo

Kwaupande mwingine Mhe Ringo amewaonya wananchi ambao wanajenga uzio na kuziba mitaro ya maji kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwani wao wanasababisha adha ambazo hazina sababu kwa kuzuia maji kutopita katika njia zake za hasili na kujaa katika maeneo ya makazi ya watu au kujaa katika barabara.