Dodoma FM
Dodoma FM
18 February 2026, 4:55 pm

Changamoto na mapendekezo yao kwa haraka zaidi, huku mifumo ya kidijitali ya ufuatiliaji ikihakikisha mawasiliano yanakuwa ya wakati na yenye tija.
Na Yussuph Hassan.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeimarisha Dawati la Huduma kwa Wateja pamoja na mifumo ya ufuatiliaji wa watoa huduma, hatua inayolenga kuongeza uwazi, ufanisi na ushirikishwaji mkubwa katika maamuzi ya sekta.
Hayo yameelezwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji (ABC 2026) uliofanyika jijini Dodoma, ambapo alifafanua kuwa maboresho hayo yanatoa fursa kwa watoa huduma kushiriki kikamilifu katika michakato ya maamuzi na utoaji wa maoni.
Dkt. Bakari alisema kuwa kupitia Dawati la Huduma lililoboreshwa, wadau wanaweza kuwasilisha hoja, changamoto na mapendekezo yao kwa haraka zaidi, huku mifumo ya kidijitali ya ufuatiliaji ikihakikisha mawasiliano yanakuwa ya wakati na yenye tija.