Dodoma FM

Wafanyabiashara watakiwa kuzingatia sheria matumizi ya leseni

18 February 2026, 4:31 pm

Picha ni Rehema Kionaumela afisa leseni mwandamizi kutoka Brela wakati  akizungumza na Taswira ya Habari.Picha na George John.

Afisahuyo amesisitiza juu ya suala  la kuzingatia sheria zote zinazo husu ufanyaji wa biashara ili kuwapa uwanja mpana wakufanya biashara zao kwa uhuru.

Jerome John.

WafanyabiasharaMkoani Dodoma watakiwakuzingatia suala la leseni za biashara zao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wito huoumetolewana Rehema Kionaumela afisa leseni mwandamizi kutoka Brela wakati  akizungumza na Taswira ya Habari,amebainisha kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wanashindwa kuweka leseni zao sehemu ya wazi katika maeneo yao ya biashara na inasababisha wateja kushindwa kuwa na uaminifu kwao.

Aidha bi Rehema ameongeza kuwa mfanyabiashara yeyote hatakiwi kutumia leseni moja katika biashara zake tofauti nikinyume cha sheria na hatua zaidi zinaweza kuchukuliwa endapo akibainika kufanya hivyo.

Sauti ya Rehema Kionaumela