Dodoma FM

Wanafunzi Ihumwa wahimizwa kusoma kwa bidii kabla ya mitihani

17 February 2026, 4:33 pm

Wanafunzi wapatao 212 walio fanya mitihani wa kidato Cha nne mwaka Jana wamefanikiwa kupata ufaulu wa madaraja manne kati ya 216.Picha na Michuzi.

Wanafunzi wapatao 212 walio fanya mitihani wa kidato Cha nne mwaka Jana wamefanikiwa kupata ufaulu wa madaraja manne kati ya 216 Ambapo waliopata daraja la kwanza ni 18,daraja la pili 55,daraja la tatu wakiwa 43 na Daraja la nne wakiwa 96.

Na Victor Chigwada.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Ihumwa wamepewa nasaha ya kuhakikisha wanajianda vyema na masomo yao kabla ya kuingia kwenye mitihani.

Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa shirika la FAWE nchini Bi.Cheka omary ikiwa shirika Hilo ni miongoni mwa wadau walio azimia kuleta mabadiliko chanya katika  shule hiyo ikiwa ni pamoja na maboresho ya majengo ,ujenzi wa vyumba vya mabweni sanjari na uzio wa shule hiyo.

Bi.Cheka Omary ameongeza kuwa kufanya mtihani wa mwisho haina maana hatima ya maisha ya mtu imeishia hapo bali zipo njia zingine za kuhakikisha wanakuwa na maisha bora

Sauti ya Bi.Cheka Omary .

Nao baadhi wanafunzi wa shule hiyo wameipongeza Serikali Kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya shule kuwapa kipaumbele watoto wa kike ambao awali walionekana hawawezi

Sauti za wanafunzi.