Dodoma FM

Ving’awe waiomba serikali kutimiza ahadi ya kuwapatia maeneo

17 February 2026, 3:27 pm

Kero hiyo imekuwa ya muda mrefu ,huku wakiendelea kupewa maneno bila utekelezaji wowote .Picha na Steven Noel.

Kwa upande wake mtendaji  wa Kijiji hicho Bi. Rehema Kihimba amesema wameanza kupanda miti kwenye eneo hilo ili kuzuia mmomonyoko .

Na Steven Noel.

Wananchi wa kata ya Vig’hawe  mtaa wa majengo na hazina wameiomba serikali kutimiza ahadi ya kuwapatia viwanja kama walivyo  ahidiwa  Ili kuweza kupata makazi mengine baada ya awali kusombwa na korongo la shabani Robert miaka tisa iliyopita.

Wakizungumza na chombo hiki baadhi ya Wananchi wamesema  kero hiyo imekuwa ya muda mrefu ,huku wakiendelea kupewa maneno bila utekelezaji wowote .

Frank Ngubes na Ruth Daud  ni wakazi wa mtaa wahazina wamesema

Sauti ya kina .

Naye katibu mwenyezi wa chama cha mapinduzi bwana Omary Mstafu  amekili kupokea changamoto hiyo na kuipelekeka ngazi za juu Kwa utekelezaji.