Dodoma FM

Vijiji 80 vyapimwa kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji  

16 February 2026, 4:31 pm

Picha ni Waziri wa kilimo Daniel Chongolo Akizungumza wakati wa ziara ya Waziri Mkuu mkoani Tanga.Picha na Kitana Hamis.

Moja ya chanzo kikubwa cha migogoro hiyo ni baadhi ya wafugaji kuhama mara kwa mara wakitafuta malisho.

Na Kitana Hamis.

Waziri wa kilimo Daniel Chongolo amesema bado kuna changamoto ya migogoro kati ya wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga licha ya hatua mbalimbali  zinazochukuliwa na Serikali kupunguza tatizo hilo.

Akizungumza wakati wa ziara ya Waziri Mkuu mkoani humo Chongolo amesema tayari Serikali imepima vijiji 80 kati ya 91 na kupanga matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo maalum ya kilimo na marisho, hatua inayolenga kumaliza kabisa migogoro hiyo ya muda mrefu.

Amesema moja ya chanzo kikubwa cha migogoro hiyo ni baadhi ya wafugaji kuhama mara kwa mara wakitafuta malisho, hali inayosababisha kuvamia maeneo ya wakulima jambo ambalo limepelekea Serikali kuongeza kasi ya kuwaandikisha wananchi kwenye daftari la makazi ili kudhibiti uhamaji holela na kuweka utaratibu rasmi wa makazi.

Katika hatua nyingine, Waziri Chonholo amesema Mkoa wa Tanga umeendelea kufanya vizuri kwenye uzalishaji wa chakula ambapo katika msimu uliopita wa mavunk umevuna tani 909,668 za mazao ya chakula wakati mahitaji ya mkoa huo kwa mwaka ni tani 762,921 pekee.

Amesema hali hiyo imeufanya mkoa huo kuwa na ziada ya takribani tani 146,000 za chakula, ziada ambayo imechangia kuimarisha akiba ya Taifa na kusaidia nchi kuendelea kujitosheleza kwa chakula.

Kuhusu zao la mkonge, Chongolo amesema changamoto kubwa inayowakabili wakulima ni ukosefu wa miundombinu ya uchakataji, jambo ambalo limeifanya Serikali kutoa Shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kujenga kituo cha uchakataji wa mkonge katika Wilaya ya Handeni, hatua itakayoongeza thamani ya zao hilo na kuongeza kipato kwa wakulima.

Sauti kina