Dodoma FM
Dodoma FM
13 February 2026, 4:52 pm

Mwenyekiti amesema wanajipanga kuanzisha mpango wa kuchangia ujenzi wa shule shikizi itakayo saidia kupunguza umbali Kwa vitongoji viwili.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa kitongoji cha Mabwe Kijiji Cha Chiona Wilayani Chamwino wameiomba Serikali kuanzisha kwa ujenzi wa shule shikizi ili kuwaepusha watoto wadogo kutembea umbali mrefu wanapo kwenda shuleni.
Wamesema kuwa kila siku watoto hao wanalazimika kutembea kilomita nne hadi shule ilipo hali ambayo ni kufuata huduma ya shule ilipo.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji Cha Chiona Bw.Vincent Chilewa amekiri uwepo wa changamoto hiyo Kwa watoto wadogo kutembea umbali mrefu.