Dodoma FM

Posta kutumia wataalam wa lugha za alama

6 February 2026, 12:48 pm

Hatua hiyo inalenga kuboresha mawasiliano na kuondoa changamoto ya kutokuelewana inayojitokeza.Picha na Anwary Shaban.

Hatua ya Shirika la Posta Tanzania kuanza kutumia  wataalam wa lugha ya alama inatajwa kuwa mfano wa kuigwa kwa tasisi  zingine za umma katika kuhakikisha haki ya kupata huduma inazingatia kila mwananchi bila ubaguzi.

Na Anwary Shaban.

Shirika la Posta Tanzania limepanga kuanza kutumia wataalam wa lugha za alama katika vituo vyake vya huduma nchini ikiwa ni sehemu ya  juhudi za serikali kuhakikisha watu wenye mahitaji maalumu hawabaki  nyuma katika maendeleo ya huduma za kidigitali.

Hatua hiyo inalenga kuboresha mawasiliano na kuondoa changamoto ya kutokuelewana inayojitokeza pale wateja viziwi wanapofika kupata huduma katika vituo vya posta.

Akizungumza na wataalamu wa anuai za jamii kutoka ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, meneja wa shirika la posta mkoa wa Dodoma Dongwe Dongwe amesema uwepo wa wataalam  wa lugha ya alama utaongeza ufanisi, usalama na usawa  katika utoaji wa huduma.

Sauti ya Dongwe Dongwe .

Ameeleza kuwa kabla  ya kuanza rasmi kwa matumizi ya wataalam hao shirika hilo litatoa mafunzo  kwa watumishi  wake kuhusu  namna sahihi ya kuhudumia watu wenye ulemavu .

Sauti ya Dongwe Dongwe .

Kwa upande wake mkurugenzi msaidizi wa anuia za jamii kutoka ofisi ya Rais Menejimenti  ya utumishi wa umma na utawala bora Mwanaamani Mtoro amesema serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha huduma za kidigitali zinafika kwa makundi yote ikiwemo watoto ili kuwajengea uwezo wa matumizi sahihi ya teknolojia wakiwa katika umri mdogo.

Sauti ya Mwanaamani Mtoro .

Nae mshauri muelekezi wa mradi wa DTP Caroline  Ndosi amesema mradi huo unaunga  mkono jitihada zote zinazolenga kujenga mifumo jumuishi ya huduma za umma kwa kutumia teknolojia rafiki kwa makundi yoyote ya kijamii.

Sauti ya Caroline  Ndosi