Dodoma FM
Dodoma FM
5 February 2026, 5:06 pm

Kwagilwa ametoa kauli hiyo bungeni Jijini Dodoma, akijibu maswali ya wabunge kuhusu utoaji wa mikopo hiyo.
Na Mariam Kasawa.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Reuben Kwagilwa, amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri na maafisa maendeleo kote nchini kuwafuata watu wenye ulemavu pale walipo badala ya kuwasubiri wafike ofisini kuomba mikopo ya asilimia 10.
Aidha, amesema serikali imetenga fedha kwa ajili ya kununua vifurushi vya simu kwa maafisa maendeleo ya jamii, ili kuwasaidia kuwafikia wanufaika wa mikopo hiyo hadi vijijini.