Dodoma FM

Mpwapwa wakabidhi mkopo wa shilingi Milioni 228 Kwa Wanawake na Vijana

4 February 2026, 11:36 am

Picha nimwenyekiti wa halmashauri hiyo mhe Richard Maponda akiongea na wanufaika hao wa mkopo.Picha na Steven Noel.

Mala baada ya halmashauri hiyo Kutangaza dilisha la mkopo walipokea maombi ya zaidi ya bilioni Moja kitu kinakinacho ashiria kuwepo Kwa uhitaji mkubwa wa mkopo huo Kwa Jamii.

Na Steven Noel.
Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma imekabithi jumla ya mkopo wa shilingi Milioni 228 Kwa makundi ya wanawake na vijana .

Akiongea wakati wa kukabithi mkopo huo mwenyekiti wa halmashauri hiyo mhe Richard Maponda amewataka wanufaika hao kutumia mkopo huo Kwa malengo yaliyo kusudiwa.

Aidha amesema miongoni mwa mpango wa taifa wa kupunguza umaskini Kwa makundi maluum ambao vi wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ,ni kutoa mikopo hiyo ambayo halmashauri hupimwa Kwa kutekeleza mpango huo.

Kwa upande wake Afisa maendeleo ya Jamii bwana Bahati Magumula amesema mkopo huo umewanufaisha makundi 32 ambayo ni watu 249 ikiwa wanawake 183 na vijana 66 ambao wamenufaika na mkopo huo.

Naye Mbunge wa Mpwapwa Mhe George Nathan Malima nae amehimiza wanafaika hao kutumia mkopo huo Kwa jinsi serikali inavyo kusudiwa kuyakwamua makundi hayo kiuchumi na kuachana na mikopo ya kausha damu ambayo imeonyesha matokeo hasi Kwa Jamii ikiwemo baadhi ya akina mama kusababisha ndoa kuvunjika .

Wakati kaimu Afisa tawala wilaya bwana Obert mwalyego amesema serikali haitasita kuchukua hatua Kwa wale wote watakao kwamisha kuto kulipa mkopo huo na kukwamisha mzunguko wa mkopo kushidwa kuendelea.

Baadhi ya wanufaika wa mkopo huo ambao ni vijana na wanawake walitumia fursa hiyo kutoa shukrani Kwa serikali kuweza kuwasaidia na kuwakwamua kiuchumi.