Dodoma FM
Dodoma FM
27 January 2026, 4:49 pm

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wamepata nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo yao kuhusu bajeti hiyo, wakisisitiza umuhimu wa kuzingatia maslahi ya watumishi pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ili halmashauri iweze kutekeleza mipango yake kwa ufanisi.
Na Lilian Leopold.
Katika mwaka wa fedha 2026/ 2027 halmashauri ya jiji la Dodoma imekadiria kukusanya jumla ya shilingi bilioni 166 kutoka vyanzo vyake vya ndani, serikali kuu na wahisani mbalimbali kwaajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo, utoaji huduma na kujiendesha.
Hayo yamezungumzwa na Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Francis Kaunda katika kikao cha kujadili utekelezaj wa shughuli za halmashauri na Baraza la Wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Naye, Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma,Dennis Gondwe amesema kuwa baraza linaunga mkono jitihada za uongozi katika kuandaa bajeti inayozingatia vipaumbele vya maendeleo na maslahi ya watumishi.
Kwa upande wake, Katibu TALGWU Mkoa wa Dododoma, Audax Stephen amewataka watumishi kuhakikisha wanafanya usimamizi madhubuti wa fedha za umma na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya matumizi ya fedha ili kuepuka hoja zisizo za lazima katika ukaguzi.