Dodoma FM

Johari aapishwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali

5 November 2025, 4:35 pm

Picha ni Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) akiapa leo ikilu Chamwino.Picha na Ikulu.

Johari ameapishwa baada ya kuteuliwa na Rais Samia Novemba 3, 2025, saa chache baada ya Samia kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania.

Na Yussuph Hassan
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemwapisha Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Johari ameapishwa leo Jumatano, Novemba 5, 20254, Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi.

Johari ameapishwa kuendelea na wadhifa huo baada ya kuteuliwa kwa mara ya kwanza Agosti 15, 2024 kuchukua nafasi ya Dk Eliezer Feleshi ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Sauti ya Hamza Johari.