Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuzingatia chanjo ya polio kwa watoto

21 August 2025, 4:33 pm

UNICEF inahimiza kila nchi kuhakikisha Watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 wanapatiwa chanjo.Picha na Google.

Hivi karibuni UNICEF na shirika la afya duniani WHO nchini Tanzania walizindua kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio iliyowafikia Watoto zaidi ya milioni 4.

Na Lovenes Miriam.
Wazazi hususani wanawake wametakiwa kuachana na tabia ya kudharau chanjo ya polio ili kuwalinda Watoto wao dhidi ya ulemavu wa kudumu.

Shirika la umoja wa mataifa la kudumu UNICEF linahimiza kila nchi kuhakikisha Watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 wanapatiwa chanjo dhidi ya polio ugonjwa ambao sio tu unasababisha ulemavu kwa Watoto lakini pia kukatili maisha yao.

Wito huo unafuatia tabia iliyokithiri kwa baadhi ya wazazi kutomaliza sindano zote nne za chanjo hiyo huku wataalamu wa afya wakieleza madhara ya kufanya hivyo.

Sauti ya Dkt.

Baadhi ya wananchi wanasema elimu ya chanjo ya polio ni muhimu kwa jamii hususani kwa akina mama ambao mara nyingi hupuuza chanjo hiyo kutokana na kutokuelewa madhara yake.

Sauti za wazazi.