Dodoma FM
Utandawazi chanzo cha ufahamu kwa mtoto
6 November 2024, 5:53 pm
Na Lilian Leopold.
Mitandao ya kijamii imetajwa kuwa ni moja ya chanzo kikubwa cha ufahamu watoto wa kitanzania kujifunza mambo mbalimbali.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wazazi mkoani Dodoma ambapo wamesema kuwa mitandao ya kijamii ikitumiwa vizuri itawasaidia watoto kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo ya kidini na kielimu.
Sanjari na hayo wameshauri jamii kuwa inawapasa wazazi kuwa karibu na watoto na kuwasimamia wakati wanapotumia mitandao ya kijamii katika mafunzo yao ili kuepuka kutumia mitandao hiyo kufanya mambo yasiyofaa.