Waliompiga Ismail Wabu wako wapi?
4 November 2024, 7:34 pm
Na Steven Noel.
Bwn. Ismail Wabu kwa Afisa Afya wa Wilaya ya Mpwapwa anayeishi Mtaa wa Hazina Mkwatani Wilayani Mpwapwa yupo kitandani kwa zaidi ya miezi mitatu akiwa amepooza kutokana na kupigwa na wananchi akiwa katika majukumu yake ya kikazi.
Bwn. Ismail Wabu alipata madhila hayo wakati akihamasisha matumizi bora ya choo ili kuepuka magonjwa ya mlipuko katika kijiji cha Igoji Wilayani Mpwapwa kama anavyoeleza Kaimu Mganga Mkuu Bwn. Charles Kaswiza.
Aidha Mpya wa Bwn. Ismael Wabu Ndg. Issa Mnamo anaeleza jinsi hatua za kisheria zilizochukuliwa baada ya tukio hilo.
Jitihada zilizofanyika za kufika katika ofisi ya polisi mpwapwa ili kupata kujua hatima ya waliofanya ukatili huo hazikuzaa matunda kwani baadhi ya maofisa wa polisi waliokuwepo kwenye ofisi hiyo walisema kuwa wao siyo wasemaji wakuu.