Dodoma FM

Viongozi wa dini watahadharisha jamii uamuzi wa kujiua

25 October 2024, 6:36 pm

Na Nazael Mkude.

Viongozi wa dini  jijini Dodoma wametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujitoa uhai kutokana na changamoto za maisha.

Wakizunguzma kwa nyakati tofauti, viongozi  hao wa dini wamesema ni dhambi mbele za Mungu kuchukua maamuzi ya kujiua.

Pichani Sheikh Hashimu Seif kutoka Masjid Shalihima Chinangali Dodoma
Sauti ya Sheikh Hashimu Seif

Viongozi hao wa dini wameeleza kuwa  binadamu wanapaswa kuishi kuwa na hofu ya Mungu kila kunapokucha kwa lengo la kutenda mema ili kujiwekea hazina ya peponi.

Pichani Mchungaji Eliya Timotheo kutoka Kanisa la FPCT Chamwino
Sauti ya Mchungaji Eliya Timotheo

Viongozi hao wa dini wametahadharisha hayo kufuatia na mfululizo wa matukio ya watu kujinyonga katika baadhi ya maeneo jijini Dodoma.