Dodoma FM
Madini yapata vitendea kazi kudhibiti upotevu
21 October 2024, 7:35 pm
Na Mariam Kasawa.
Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amezindua magari mapya 25 yalilyotolewa na serikali kama vitendea kazi ili kutimiza lengo la makusanyo ya mapato na udhibiti wa utoroshaji wa madini.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, octoba 21 Mhe. Mavunde amesema kuwa magari hayo ni kwa ajili ya mpango wa uboreshaji wa usimamizi wa Sekta ya Madini.
Aidha Mhe. Mavunde ameelekeza magari hayo yafungwe GPS kwa ajili ya kuangalia mwenendo wake ili kuhakikisha yanatumika katika matumizi yaliyokusudiwa.